kurudi mwanzo

Atoa onyo kwa vijana
Na David Ogot Kenya Leo 6th. September 1989

WANAYUSI wa KANU fulani na maafisa wengine ambao huwa na tabia ya kuwatahadhirisha wauza pombe ya chang'aa wakati wanapokaribia kuskwa watachukuliwa hatua kali. Onyo hilo limetolewa na mwenyekiti wa Kanu tawi la Soi katika Wilaya ya Uasin Gishu, Bw Joel Sirma.

Akioengea na mwandishi wetu, Bw. Sirma alisema watu hawa wachache wanaharibu jina nzuri la wengine wote ambao wamejitahidi kuangamiza pombe hiyo haramu tangu Rais moi atoe agizo la kupambana na uovu huo.

Alisema ni vigumu kuangamiza pombe hiyo iwapo kila wakati polisi wanayusi wanapojiandaa kwenda kusaka mahali, hugundua kwamba tayari watu wa sehemu inayohusika huwa wamejua mapema.

Aliwashauri wanayusi washirikiane na maafisa wa polisi pamoja na watawala katika kuangamiza kabisa maovu yote. Alimpongeza Rais Moi kwa kutoa agizo la kungamiza pombe ya chang'aa na pombe nyingine siziso halali pamoja na madawa ya kulevyia.

Kurudi mwanzo


Mtandao huu umetengenezwa na David Ogot snr. na unadumishwa na
Science & Engineering Research Center
©goinghomedotcom 2001 - 2006
Disclaimer Privacy Policy