| Mawazo na Istilani Muhimu |
|---|
| Kiswahili - English Glossary |
| This list is by no means exhaustive. If you have any terms you would like us include, please send them to us. |
Dalili za ugonjwa: Ni orodha ya sifa bainifu au dalili ambazo mteja anaweza kuwa nazo za kuonyesha hali ya ugonjwa fulani
Kujinasua: Kwa mtu mwenye utegemezi wa kileo, ni lazima atumie kileo ili aweze kukubaliana na maisha na kutekeleza kazi zake za kawaida. Wakati kileo hakitumiwi, mtu huyo huumia kimwili na kiakili hali iitwayo dalili za kujinasua. dalili za kimwili za kujinasua na heroini, kwa mfano, hudumu kati ya siku tatu hadi saba.
Kujiyima: Hali ya kutokunywa au kutumia dutu. Mtu ambaye henywi pombe anajinyima pombe. Wakati mtumiaji vibaya wa vileo, hasa baada ya matibabu, anaacha kuvitumia vileo kabisa, basi amejinyima
Kuondoa sumu ('Detox') Hii ni tiba ya utegemezi wa kileo mwilini. Mtumiaji wa madawa hukubali kutunza kwa kulishwa kwa chakula bora, kutibiwa na kupewa vitamini mpaka dalili za kujinasua zimalizike. Utabibu huweza kuhusisha upungufu wa polepole wa kiasi na mazoea ya utumiaji wa madawa hayo au utumiaji wa muda kibadala cha madawa hayo au utumiaji wa muda wa kibadala cha madawa ya kelevya, kilichokubalika katika mpango wa tiba. maji yenye chumvi na sukari hupewa mteja aliyepungukiwa na maji mwilini. Wateja wengi huhitaji kula vitamini na madini ya kujenga mwili ili kurudisha afya zao.
Kurudia mwenendo mbaya: Ni wakati mtumiaji mbaya wa kileo au pombe anayepona anapoanza kutumia vileo au pombe tena baada ya kujinyima kwa muda
Kutawaliwa: mazoea ya utumiaji wa kileo huleta mabadiliko katika ubongo na mishipa ya fahamu hivyo kwamba mtumiaji huhitaji kileo hicho zaidi ili aweze kupata matokeo yanayokusidiwa. Huu ndio msingi wa kutawaliwa na kileo
Madawa ya kubadilisha akili: Madawa yenye athari ya kubadilisha akili - Madawa hayo yenye nguvu ni vileo kama LSD ("asidi") ambazo husabibisha mtumiaji kuwa na njozi au hisia za kudhania ("safari za asidi") ("acid trip")
Madawa ya kudhoofisha: Ni madawa au tiba (kama vile kitulizo) ambayo hupunguza utendaji wa mishipa ya fahamu na wa mwili wa mtumiaji. madawa ya Kudhoofisha huweza kuasibibisha kuchoka, kuuzunika na kusinzia
Mraibu (Mtegemezi wa kileo): Ni mtu ambaye amezoea kutmumia kileo na kkuza uhusiano mkubwa nacho
Mraibu anayepata afueni: Mtu ambaye amekuwa mtegemeaji sana wa kileo, anayeanzisha mtindo mpya wa maisha ya kutotumia kileo na ambaye kwa sasa hatumii vileo ("kukaa safi").
Uraibu: Uraibu ni ile tabia ya mwili na kisaikolojia au kuhisi mahitaji ambayo hutokana na kuzoea kutumia vileo. Watumiaji vibaya wa vileo mara nyingi huendelea kuhisi hamu hiyo hata baada ya kutibiwa dhidi ya utegemezi wa vileo ('uondoaji sumu')
Utegemezi: Utegemezi wa kileo ni hamu ya kihemuko na mara nyingine ya kimwili anayopata mtumiaji wa vileo. Mtumiaji mbaya wa madawa au mtegemea pombe huhisi ulazima wa kuitumia mara kwa mara, kuyasikia matokeo yake na kuepuka mateso kwa kuikosa. Utegemezi kimwili wa kileo chochote huweza kutibiwa katika mpango wa kutoa sumu (detox). Hata hivyo, utegemezi kisaikolojia ni mgumu zaidi kutibu - Hili ndilo changamoto kubwa kwako kama mshauri-nasaha
Utegemezi-wenza: Uhusinao kati ya watu wawili au zaidi ambao wanategemeana katika kutimiziana mahitaji yao hasa yale ya mihemko yenye athari mbaya
Utunzaji siri: Kule kutunza siri binafsi za mteja ambazo zimejulikana kutokana na kuhusiana naye kitaalamu. Utunzaji wa siri ni haki ya kimsingi ya mteja. hata hivyo, katika nchi zingine, mshauri nasaha anatakiwa kisheria kutoa taarifa ya ushahiddi wa mtu anayetaka kujidhuru au mwenye nia ya kujiua kwa wakuu serikalini, kwenye Mashirika ya Misaada kwa watoto au kwa Polisi.
Wingi wa raha: Hisia za kuinua mhemuko, ubashasha, kuchochewa, kulewa; furaha kubwa; huweza kuambatana na raha za kimwili. Mtu huweza kupata furaha bila kutumia kileo, kama vile furaha inayopatikana na mkimbiaji, mcheza ngoma, mwinbaji na mpenzi.
¹Source: Mwongozo wa Mashauri Nasaha wa Madawa. Mwongozo Unaofaa kwa Matumizi ya Kila Siku UNDCP Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Kimataifa wa Kudhibiti Madawa Used with permission
Back to top
Mtandao huu umetengenezwa na David Ogot snr. na unadumishwa na
Science & Engineering Research Center
©goinghomedotcom 2001 - 2006
Disclaimer
Privacy Policy