Je! Kuna Tumaini Kwa Mraibu Wa Pombe?

David Ogot snr. founder of goingdomedotcom organisation.
David Ogot snr. mwasisi na mkurugenzi wa 'goinghomedotcom'

Ninajua sasa kuwa mimi ni mraibu wa pombe. Najua kwamba siwezi kunywa tena kamwe. Siwezi kunywa katika tafrija za kirafiki, siwezi kunyua hata chupa moja au mbili tu. Kwani nikiwa mraibu wa pombe tatizo langu si kiasi cha pombe ninchokunywa bali ni pombe yenyewe. Naam tatizo langu ni kinywaji changu cha kwanza. Ninaelewa barabara kuwa usalama wangu unategemea tu kutochukua kinywaji changu cha kwanza. Lakini siwezi kuwa na kiburi wala kutosheka na maendeleo niliyoyafanya - kwani kufanya hivyo huenda kukanifanya kuteleza na juanguka tena. Kwangu mimi kuteleza ni kurudia kunywa, na kama mraibu wa pombe ninalewa vema kuwa kunyua tena ni kifo.

Lakini je? Namna gani miaka yote niliyokana uraibu wangu? Ninakumbuka vyema kabisa masaibu dhiki niliyopitia wakati huo. Sikujua kamwe kuwa nilikuwa mraibu wa pombe. Mke wangu, marafiki zangu, wazazi na jamaa zangu hawakujua kuwa nilikuwa mraibu wa pombe.

Sikujua ni nini kilichokua kninanipata wakati huo. Nilijua nilikua na tatizo lakini tatizo gani? Je! Nilikuwa ninapata kichaa (wazimu)? Mbona niliendelea kufanya mambo ya kusikitisha ambayo yaliwaumiza sana wapendwa wangu? Ni ahadi ngapi nilizokuwa nimewavunjia? Je wazimu huu ungeisha? Lazima ungeisha! lakini uliisha kwa muda mfupi tu, hadi niliporudia tena.

Eileen Mlamba-Ogot  co-founder of goingdomedotcom organisation.
Eileen Mlamba - Ogot mwasisi-mwenzi na mkurugenzi wa 'goinghomedotcom'

Nilihisi kuwa na hatia ambayo singeweza kstamilihili. Mawazo ya kujitia kitanzi (kujiua) yalinijia akilini mara kwa mara. Niliwahi kujaribu 'suluhisho" hili pindi moja nilipokuwa masomoni nchini India. Ilimbidi mama yangu mwenye uvumilivu sana kuja mara moja alipoarifu kwa telegram kuwa nilikuwa katika hali mahututi huku kifo kikinitambulia macho. Lakini niliishi japo nalishangaa kama kweli ningeeendelea kuishi na hatia hii tena?

Mkondo wangu wa maisha ulikuwa kama ule wa waraibu wengine wanaoendelea kunywa. Utu wangu ufahamu wangu ulikuwa umebadilika sana hivi kwamba singeweza kutumia uwezo vipawa vyangu tena.

Heshima yangu iliharibiwa kabisa hivi kwamba nilijificha katika vituo vya chang'aa na kujitokeza kwa marafiki wangu wakati tu nimelewa chakari. Nilipoteza kazi moja baada nyingine hadi habari hizi zikaenea mno na kupelekea waajiri kukataa kabisa kuniajiri tena. lakini si kwamba nilijali tena. Kufanya kazi ilikuwa ni kupoteza wakati tu. Kulikuwa na njia rahisi zaidi za kupata pesa kama vile kudanganya marafiki, kuuza vifaa vya nyumbani kutoka kwangu au kwa wazazi wangu, kuazima pesa (bila kulipa) na hata kuiba wakati mwingine.

Nilijipata matatani na polisi mara kwa mara hasa baada ya kunywa katika mojapo ya hoteli kubwa jijini na kujaribu kutoroka bila kulipa. Hizo ndizo zilikuwa sehemu pekee ambazo ungeweza kunywa bila kulipa kwanza kama ulikuwa na ujasiri wa kutosha. Nilianza kushuka moyo na kuigiwa na hangaiko wa wasiwasi mkubwa.

Watoto wangu walifedheheshwa nami na marafiki zangu kuniepuka kutokana na tabia yangu ya kuudhi, lakini bado niliendelea kunywa. Mke wangu aliekea kukata tamaa, alitisha kuondoka mara kadhaa lakini nilimsihi abaki. na bado niliendelea kunywa.

Nililazwa hospitalini mara kwa mara, lakini kwa sababu ilikuwa ni kutokana na niumonia (kichomi) au maradhi mengine ya mapafu hakuna aliyehusisha maradhi hayo na pombe, na bado niliendelea kunywa. Nilipatwa na ajali, nilihusika katika vita hata kupata ajali mbaya ya pikipiki nilipokuwa India ambapo niliponea chupuchupu na kupoteza mena kadhaa pamoja na kuvunjika goti. Lakini nikiwa na plasta mguuni na uso uliovimba kama kibofu bado nilimudu kutumia mrija-kunywa pombe!

Na je! kama niingeendelea hivyo? Mkondo wangu wa maisha ungekuwa kama ule ambao umepitiwa na mamilioni ya watu ambao wameanngamia kabla yangu. Ini langu, moyo wangu, na mfumo wangu na neva ungeharibika na ningelazwa tena nikiwa na maradhi mabaya zaidi yanayohusiana na pombe. Labda ningejiua (ningejitia kitanzi) ama ningeangamia katika mojapo ya ajali

Ama labda ningekufa kutokana na kutiwa sumu na pombe mwilini, maradhi, kuchomeka kwa ini, maradhi ya moyo au ya mapafu. na ulimwengu ungepotoshwa kutokana na cheti changu cha kifo kuonyesha kuwa sababu ya kifo changu ilikuwa ajali, moto (baada ya kulala na sigareti ilowashwa) kujiua, maradhi ya moyo au ya ini. Labda hata daktari wangu hangetanbua vyema Kisa na maana ya kifo changu, yaani uraibu wa pombe.

Lakini baada y kutambua waziwazi kuwa nilikuwa mraibu wa pombe jamaa yangu nami hatukujua la kufanya. Je! Kulikuwa na mahali popote pa kwenda? Je! Nilikuwa na nafasi yoyote? Ilikuwa viguma sana. Lakini yote yangewezekana

Kulikuwa na mapendekeo ya kila aina, na kwa takibanb miaka huku na huku na kila mara nikarudia kunywa. Hakimaye nilikata tamaa. Je! Kulikuwa na tumanini lolote?

Lakini hatimaye nilifika mahali ambapo palinipa tumaini halisi. pahali paliponitia katika mkondo wangu wa kupona. Ni wakati nilipokuwa karibu kuondoka katika kituo hiki ambapo mawazo yaliyoniongoza baadaya kuanzisha goinghomedotcom yalinijia

Nilihitaji kuwahamisisha umma kwa ujumla kuhusu uraibu wa pombe. Na kuwahamisisha katika lugha rahisi sana bila mjadala wa kama uraibu huo ni ungonjwa au la, mbinu bora zaidi za kuutibu na khadhalika. Nilichotaka tu ilikuwa kuwajulisha familia zote kitu kimoja, kuwa uraibu wa pombe ni ugonjwa na kuwa kuna tumaini.

Kwa wazazi, vijana, wake au akina mama, waume au marafiki-naam kuna tumaini!!!

Nachukia ugonjwa huo sasa wala sijichukii. Ukiwa na mpendwa wako ambaye ana uraibu wa pombe, usimchukie. Uchukie ugonjwa. Lakini usife moyo na kukata tamaa. Kuna tumaini. Ugonjwa huu unuaweza kutibiwa. Tofauti na magonjwa mengine ya kufisha mpendwa wako anaweza tena kurudia maisha yake kawaida na yenye kunufaisha jamii.

Natumaini mtandao huu utawasaidia nyote mnaotumia, iawe una tatizo la pombe (au dawa nyingine za kulevya) au la. Kwani ikiwa utamsaidia hata mtu mmoja tu kurudia maisha yake ya kawaida kama nilivyofanya, basi itatosha.

Asante kwa kunipa muda wenyu na kusoma habari hii. Mungu na awabariki.

David Ogot snr.
4th. May 2001

Kumbuka: mtandao huu ni kama matibabu, hubadilika daima.

Kurudi mwanzo


Mtandao huu umetengenezwa na David Ogot snr. na unadumishwa na
Science & Engineering Research Center
©goinghomedotcom 2001 - 2007
Disclaimer Privacy Policy