| goinghomedotcom ni nini? |
|---|
Mtu asemapo 'anakwenda nyumbani' picha na hisia za usalama, joto la upendo, starehe na kukubaliwa na jamii huzuka. Kizibio kutoka janga zinazojulikana na zisizojulikana, ambazo ni afadhali ziachwe pale ambapo haziwezi kudhuru; nje! katika familia za kawaida mawaidha yoyote anayopata ni ya kukusaidia na kukusalimisha dhidhi ya janga mbalimbali. katika familia bora kila mtu hujali masilahi ya wale wengine wasije wakapata maafa yoyote. Hivyo basi nymbani ni kwnye furaha na amani.
Maelfu ya wananchi Wakenya, vijana kwa wazee, wamepotoshwa au wako karibu kupotoshwa kwa sababu ya janga la unywaji wa pombe na matumizi ya madawa za kulevya. Wengi wa Wanakenya hawa wamekaribia kupoteza maisha yao. Nchi yetu inalia; ghasia kwenye mashule pamoja na vifo vya watu wengi kwa wakati mmoja, ubakaji, majaribio ya ubakaji na uharibifu wa mali ya mashule vimekuwa vitendo vya kawaida vinavyofanywa na vijana waliolewa pombe na madawa ya kulevya.
Isitoshe, kuongeza uovu wa janga hili maradufu ni maenezi ya ugonjwa anaosabibisha kifo - UKIMWI. Je, tunangoja nini? Tumekawia sana kufanya jambo ili kutatua janga hili linalozorotesha kwa kasi ilhali kilio cha kutuhamasisha kimekuwepo muda mrefu.
Inatubidi turudi kwenye wakati wa ustaarabu. Wakati ambapo matumizi ya madawa ya kulevya haukujulikana sana na unywaji na idhini ya kunywa pombe, na unywaji wa pombe kwa wingi ulishutumiwa. wakati ambapo vijana wangeweza kustarehe bila kunywa pombe au kutumia madawa ya kulevya. Tunahitajika kutupilia mbali hizi 'janga picha' za unywaji wa pombe na utumiaji wa madawa ya kulevya: tunahitaji kwenda nyumbani.
Jina 'goinghomedotcom' imezuka kutokana na ukweli kuwa 'nimerudi nyumbani' kuwa yule muu niliyekuwa kabla sijaanza kunywa pombe. Nilikuwa nje kwenye baridi, pombe ilikuwa imenirusha nje ya nyumba yangu, lakini sasa nimerudi nyumbani. Ninataka vijana wetu waurdi nyumbani pia. Sehemu ya 'dotcom' ya jina 'goinghomedotcom' inarejelea ukweli kuwa kizazi cha wakati huu cha vijana kimepewa jina 'kizazi cha dotcom'. Kizazi hiki ndicho ninachokusudia ujumbe huu kwa kiwango kikubwa. Pia ninatumia mtandao na njia nyingine kisasa ambazo zinaendelea kuibuka, zinazojulikana kama teknolojia ya dotcom ili kuwasilisha ujumbe wangu.
Kwa nini 'goinghomedotcom' imeendelezwa kwa herufi ndogo ya 'g'? Hii ni kwa sababu msaada huu hautuhusu sisi bali unakuhusu wewe. Sisi tuko hapa kukutumikia kwa unyenyekevu. Ujumbe huu si kunihusu mimi, bali unakuhusu wewe. Niliamka kutoka ndoto yangu mbaya kwa sababu mtu fulani alinipatia wakati wake, kunizungumzia bila kukata tamaa ya kubadilikia kwangu. Mimi nawapatia wengine nilichopewa kutumia na kuendeleza.
Hadhira ya Wakenya haijangundua uzito wa janga la unywaji wa pombe na utumizi wa madawa ya kulevya kote nchini. Pombe hasa, haieleweki kama dawa ya hatari. Unywaji wa pombe kwa wingi na vinwaji vingine vinavyoweza kkulewesha wakati wowote na pahali popote, unaangaliwa kama tu starehe zisizodhuru.
'goinghomedotcom Trust' imeandikishwa katika Nchi ya Kenya kama muungano wa kusaidia jamii. Lengo la muungano huu ni kujilisha watu kote nchini (na pia Afrika yote) kuhusu hatari za pombe na dawa zingine na pia kuwapa Wakenya motisho ya kutaka kujifunza mengi juu ya jambo hili. Imesemekana kuwa ujuzi ni nguvu. Hatuhitaji mashirika mekubwa na mamilioni kupigana na janga hili. Tunachohitaji ni ujuzi tu! Unapojifunza juu ya pombe na dawa zengine, halafu ufunze jamaa yako, mara moja nchi huelimika. Nchi iliyo na ujuzi ni nchi iliyo na uwezo. Jichunge na Jifunze! 'goinghomedotcom Trust' inakusudia kuhamasisha mwenendo mpya wa maisha katika nchi yetu ya Kenya, hasa kati vijana. Mwenendo huu wa maisha utawaonyesha vijana kwamba kuwa 'high' au kulewa ni jambo la zama na kutolewa ndio maisha ya kisasa.
'goinghomedotcom Trust' inakusudia kufanya jambo hili kwa kuwahusisha vijana ili waone hatari iliopo, waone kuwa hakuna haja ya kukunywa pombe na kutumia dawa ya kelevya na wagundue hatari ilioko katika pombe na dawa zingine.
Ni lazima vijana wagundue kuwa kwa kutumia pombe na dawa zingine vibaya wanajiweka kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa UKIMWI au virusi ya HIV. Vijana pia wanapaswa kujua kuwa janga hili wa UKIMWI na HIV inaharibu, bila huruma, maisha ya mamia ya vijana kila siku na kwamba ni lazima kuwe na marekebisho ya mawazo ambayo yataleta mabadiliko ya tabia. Ni kwa njia hii tu ambapo ujuzi waliopata utakuwa na manufaa.
'goinghomedotcom Trust' pia itasaidia wale ambao wanateseka kwa sababu ya unywaji wa pombe na matumizi ya madawa ya kulevya kupata ujumbe na mawaidha yote kuhusu hali yao, mahali ambapo wanaweza kupata usaidizi na pia matokeo ya kutopata usaidizi. Ujumbe huu wote umeandikiwa katika lugha inayoeleweka na ni bure katika mtandao huu wa - www.goinghomekenya.org. Ujumbe huu wote utakuwa unapatikana kwa mtu yeyote Kenya na pia nje ya Kenya. Kwa njia hii mtandao huu utakuwa maktaba ya usaidizi muhimu kwa watu wanaoishi mashambani na kwa wanafunzi, ambao wanaweza kuchapisha ujumbe huu na kutoa nakala nyingi, ili kueneza habari hii kwa watu wengi kwa bei nafuu.
Kwa hivyo malengo ya 'goinghomedotcom Trust' ni kuleta na kuhumaisha:
Mimi kama mraibu wa pombe anayeendelea kupona, niliyepoteza miaka na pesa nyingi nikijaribu kupata mtu kunielezea kwa njia sahili shida yangu njia zilizoko za kutibiwa, ninataka watu wengine na familia zao wasipitie tabu hii kali. Bado naona walevi wengi wakipitia tabu hiyo iliyonipata, wakisukumwa kutoka pahala pamoja hadi pengine; wakati huo mabishano yakienedelea juu ya matibabu yanayoponesha na yasiyoponesha.
Wengine ni tu watu wasiokuwa waaminifu wanaotazama walevi na hali yao mbaya kama nafasi ya kupata pesa; kwa kudai aina nyingi za 'malipo' ilhali hawawapi walevi usaidizi wowote unoleta matokeo mazuri.
Wakati umewadia kumaliza unyanyasaji wa familia zilizoteseka mithili ya kwenda jehanamu na kurudi, pamoja na wanafamilia waraibu wanaopendwa sana na familia zao. Wakati umewadia kuwaambia Wakenya kuwa kuna msaada na kuwa TUMAINI ipo. Kuna uwezo wa kutupilia mazoea ya ulevi na utumizi wa dawa za kulevya.
'goinghomedotcom Trust' itajitahidi vilivyo kupinga ulaghai wa aina yoyote na uwongo wa moja kwa moja wanaoambiwa mraibu wa pombe pamoja na family zao.
Uwongo huu husambazwa na watu wanaochukua nafasi ya kujinufaisha kwa sababu ya kufa moyo na uchungu wa uraibu na familia zao. WAKATI WA KUACHA KUTESEKA NI SASA!
Kwa sababu hizi ninahisi kuwa uoni wangu wa 'goinghomedotcom Trust' umekuja wakati uaofaa sana. lakini ili uoni wangu huu ubadilike kutoka kuwa ndoto mpaka jambo halisi ni lazima tuwe na muungano wa kimawazo na tusaidiane katika juhudi hii. Tupe fursa ya kurudisha vijana wetu numbani - kwa wakati wa utulivu. Pamoja tunaweza kufanya jambo hili.
David Ogot Snr.
4th May 2001.

Mtandao huu umetengenezwa na David Ogot snr. na unadumishwa na
Science & Engineering Research Center
©goinghomedotcom 2001 - 2006
Disclaimer
Privacy Policy